Skip to main content

RC MHITA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU, AWAPA UJUMBE WANANCHI

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

RC MHITA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU, AWAPA UJUMBE WANANCHI

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Mboni Mhita, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kishapu katika   sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na unufaishaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. 

Akizungumza  katika ziara hiyo, Mhita amesema maendeleo yanayoonekana ni matokeo ya amani, utulivu na demokrasia ya kiuchumi, inayowavutia wadau wa maendeleo na wawekezaji kushirikiana na Serikali kuboresha maisha ya wananchi na kuwataka waendelee kulinda Amani na utulivu, ili maendeleo Zaidi yaweze kuonekana kwa manufaa ya jamii.



Amesema, Serikali imeendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa na kuboresha miundombinu ya shule ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya elimu katika mazingira bora, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwiano wa madarasa na matundu ya vyoo kulingana na idadi ya wanafunzi.

 Aidha, RC Mhita  amevipongeza vikundi vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, ikiwemo kikundi cha Wachapakazi kilichotumia mkopo huo kununua trekta kwa ajili ya kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji, na kuvitaka vikundi vingine vya wajasiliamali  viweze kujitokeza ili kupata mikopo hiyo inayotolewa kwa vijana wanawake na watu wenye ulemavu.

Akizungumza kwa niaba ya wanachi  Patricia Nkana  kutokea Kata katika  ya Mwataga wilayani humo  ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na upatikanaji wa maji safi na salama, akisema ujenzi na uboreshaji wa zahanati na upanuzi wa upatikanaji wa maji safi na salama umeongeza usalama wa akina mama wajawazito wakati wa kujifungua na kuinua ustawi wa wananchi kwa ujumla na kuchochea kuimarisha afya ya ndoa zao.

Kukamilika kwa miradi ya  maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ni  hatua inayolenga kuboresha huduma za kijamii na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi kwani miradi hiyo itakwenda  kuchochea maendeleo ya jamii, ikiwemo kuboresha huduma za afya, elimu, maji na miundombinu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.