Skip to main content

RC MBONI AZINDUA AWAMU YA PILI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE SHINYANGA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amezindua awamu ya pili ya mpango wa wa bia ya afya kwa watu wote zoezi lililofanyika katika uwanja wa zima moto uliopo katika manispaa ya Shinyanga.

RC MBONI AZINDUA AWAMU YA PILI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE SHINYANGA
Studio Narration JAMBO FM

RC MBONI AZINDUA AWAMU YA PILI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE SHIN...

0:00 --:--

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amezindua awamu ya pili ya mpango wa wa bia ya afya kwa watu wote zoezi lililofanyika katika uwanja wa zima moto uliopo katika manispaa ya Shinyanga.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA, MBONI MHITA

Akizungumz katika uzinduzi huo RC Mboni amewahmiza wananchi katika mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kujisajili katika mpango huo wa bima ya afaya kwa watu wote ili kupunguza gharama za matibabu pindi mwananchi anapokumbwa na changamto za kia afya

RC Mboni amesema afya ndiyo msingi wa maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla na kuanisha kuwa wananchi wa Shinyanga wanajishughulisha na kilimo ufugaji uvuvi na uchimbaji madini na kwamba ili kutekeleza shughuli hizo inaitajika wanajamii kuwa na afya njema na kuwataka kujiunga na mapnago huo ili uzalishaji kiuchumi usiweze kutetereka.

Katika hatua nyingine RC Mboni amewaagiza wakuu wa wilaya pamoja na wakurugezni katika mkoa huo kusimamia utekelezaji wa mpangu kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapatiwa elimu sahihi kuhusiana na bima ya afya kwa wote pamoja na kuhakikisha malengo ya usajili wa wananchi yanafikiwa katika maeneo yao

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi huku akianisha kuwa awamu ya kwanza ya usaji wa bima ya afya kwa watu ote ililenga kusajili wanufaika kutoka kaya za zisizokuwa na na uwezo kupitia mpango wa TASAF 14,325 ambapo kaya 11,285 zilifikiwa sawa na aslimia 78.7

Amesema awamu ya pili inalenga kufikia kaya 22065 ambazo hazikufikiwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo huku usajili wa makundi mbalimbali wakiwemo wajasiliamali ukiendelea kuwa utekelezaji wa mpango huo.

BAADHI YA WANANCHI WALIOJITOKEZA KATIKA VIWANJA VYA ZIMA MOTO MANISPAA YA SHINYANGA ILI KUJISAJILI NA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WATU WOTE

Katika mpango huo wananchi wanatarajiwa kusajiliwa kwa shilingi laki moja na nusu kwa kaya yenye ujumla ya watu sita kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika uzinduzi wa mpango huo wa bima ya afya kwa watu wote.

BAADHI YA WAHUDUMU WA AFYA WAKIENDELE NA ZOEZI LA KUSAJILI WANANCHI KATIKA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WATU WOTE

Kwa upande wake meneja wa mfuko wa bima ya afya NHIF mkoa wa Shinyanga Frankilin Chekani amesisitiza kuhusu wananchi kupata taarifa sahihi kuhusiana na mpango huo, na kuanisha kuwa mfuko wa bima ya afya kwa watu wote ni mtandao mpana katika utoaji huduma za afya kwa wananchi.

MENEJA NHIF MKOA WA SHINYANGA FRANKLIN CHEKANI

Naye afisa mipango mkuu kutoka mamlaka ya usimaizi wa bima Tanzania TIRA kanda ya magaharibi ahimidiwe Assery amsema wakiwa kama wasimamizi wa bima nchini watakwenda kusimamia huduma zinazostahili kupitia bima ya afya kwa watu wote zinatekelezwa na kuwataka wananchi kuwasilisha malalamiko katika taasisi hiyo pindi wanapoona mapungufu katika mpango huo

AFISA MIPANGO MKUU TIRA KANDA YA MAGHARIBI AHIMIDIWE ASSERY

Nao baadhi ya wanufaika wa mfuko wa bima ya afya kwa watu wote awamu ya kwanza wakapta fursa ya kueleza baadhi ya manufaa waliyopata baada ya kujiunga mfuko huo huku wakiishukuru serikali kwani kwasasa upatikanaji wa huduma za afya kwao si changamoto tena

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.