Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita amekagua miundo mbinu wezeshi katika kukabiliana na athari zinazotarajiwa kutokana na mvua za elnino, zinazotarajiwa kunyesha juu ya wastani.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MBONI MHITA
RC Mboni amekagua madaraja na mitaro inayopitisha maji katika kata za Lubaga, Ngokolo Ndembezi na Mwamalili, huku akiwataka wananchi kuendelea kuzingatia usafi katika maeneo yao ikiwemo mifereji na mazingira yanayowazunguka, ili kupunguza ukubwa wa athari zitokanazo na mvua hizo
"Taarifa za mamlaka ya hali ya hewa Tanzania zinasema mbua hiyo haijawahi kunyesha tokea miaka 150 iliyopita hivyo hakuna mwenye uzoefu na mvua hiyo itakuwa ya namna gani,hivyo hatuna budi kuchukua tahadhari kwa ukubwa ili kukabalina na mvua hiyo," amesema RC Mboni
Aidha, amesema ameridhishwa na hali ya usafi ambayo imefanyika katika mito na madaraja katika kukabiliana na athari ya mvua za elnino na kuwataka viongozi katika maeneo hayo kuendelea kusimamia zoezi la usafi ili liwe endelevu kwani mvua za juu ya wastani za elinino ndo zimepelekea usafi kufanyika kitu ambacho amesema sio sahihi.
Ameongeza kuwa, mapambano dhidi ya athari zitokanazo na mvua za elnino sio la Tarura au Tanroads pekeyake bali ni suala la kila mmoja mwenye nafai na dhamana katika eneo lake kutimiza wajibu wake kwa kusambaza elimu mpaka katika ngazi ya kaya.

RC Mboni pia amewataka wakala wa vijijini na mijini TARURA kuendelea kutengeneza mitaro katika barabara kabla ya mvua hizo pamoja na kuweka matokeo ya maji kwani barabara nyingi zinachangamoto ya kutokuwa na matokeo ya maji hali iyoweza kupelekea uharibifu wa barabara
"Tumepokea fedha nyingi sana ndani ya mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha awamu ya sita ikiwa ni shilingi tirioni mbili na zote zimekwenda kwenye miradi mbalimbali ili kutatua changamoto zinazojitokeza ikiemo miundombinu ya barabara,"amesema RC Mboni.

MENEJA WA TARURA WILAYA YA SHINYANGA SAMSON PAMPHIR
Awali akitoa taarifa juu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zitokanazo na mvua za elnino meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Samson Pampir amesema halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ina jumla ya kilomita 780.18 na kwamba wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mra katika barabara zote pamoja na kusafisha mitaro, madaraja, na makalavati.
Pamphiri amesema mpaka sasa wameshafanya kazi hiyo katika madaraja kumi ili mvua hizo zitakapoanza maji yaweze kupita kwa urahisi na kwamba wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi juu ya kufanya usafi wa mitaro pamoja na makalavati huku akianisha kuwa TARURA itaendelea kuwa karibu na wananchi katika kipindi chote cha mvua hizo ili kuzuia madhara yasijitokeze kutokana na ubovu wa miundombinu.

BAADHI YA WANANCHI WALIOJITOKEZA KATIKA ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika ziara hiyo ya mkuu wa mkoa wamesema kuwa tayari wameshapatiwa elimu na viongozi wa kiserikali juu ya kupunguza atahari zitokanazo na mvua hizo likiwemo suala la kuhama kwa muda katika maeneo yaliyo bondeni ili kupisha mvua hizo zinazotarajiwa kunyesha juu ya wastani.

BAADHI YA WANANCHI WALIOJITOKEZA KATIKA ZIARA YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MBONI MHITA

Discussion
Reader comments
0 contributions