Mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido amewataka watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba kuwajibika kikamilifu katika majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwani wanamuwakilisha Rais katika halmashauri hiyo.
Kanali Kido alisema utendaji kazi mzuri wa watumishi wa umma ni pamoja na kufanya kazi kwa umoja, kuepuka migogoro kazini hii husaidia kufikia lengo la kuwafikia wananchi kwa urahisi.

Aidha alisisitiza watumishi kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo katika halmashauri hiyo pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma kwa kutokufanya vitendo vinavyoweza kuisabishia serikali hasara.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi Mkuu wa divisheni ya maendeleo ya jamii Bi Felister Shayo aliahidi kuwa watumishi wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutimiza malengo ya serikali katika halmashauri hiyo.



Discussion
Reader comments
0 contributions