Skip to main content

RC DENDEGO AWATAKA WATUMISHI KUISHI MAENEO YA KAZI

Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanaishi katika maeneo yao ya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa urahisi na kutatua kero zao kwa wakati.

RC DENDEGO AWATAKA WATUMISHI KUISHI MAENEO YA KAZI
Studio Narration JAMBO FM

RC DENDEGO AWATAKA WATUMISHI KUISHI MAENEO YA KAZI

0:00 --:--

Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amewataka watumishi wa umma kuhakikisha wanaishi katika maeneo yao ya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa urahisi na kutatua kero zao kwa wakati.

Dendego ametoa msisitizo huo leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Singida, iliyoanzia Halmashauri ya Wilaya ya Singida, kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara. Amewataka watumishi wanaoishi mbali na vituo vyao vya kazi kuhamia katika maeneo wanayohudumu ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Baadhi ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Rodrick Mpogolo, amesisitiza kuwa pamoja na Serikali kuendelea kuboresha miundombinu na kupeleka watumishi katika maeneo mbalimbali, watumishi wanapaswa kuwahudumia wananchi kwa upendo, moyo na uadilifu ili kuhakikisha wanapata huduma stahiki.Katibu Tawala Mkoa wa Singida Rodrick Mpogolo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.