Na Saulo Stephen - Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ameshiriki Iftar na Dua maalum ya kuliombea Taifa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Hafla hiyo iliyofanyika Machi 15, 2026 katika Uwanja wa Bombadia, Halmashauri ya Manispaa ya Singida, ilihudhuriwa pia na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo Waislamu, watoto yatima, wajane na wananchi wa kawaida, wote wakikusanyika kwa lengo la kufuturu pamoja na kuombea amani na ustawi wa Taifa kwa mshikamano mkubwa.

Akizungumza katika hafla Dendego amewahimiza wananchi kuendelea kudumisha upendo, amani, kuheshimiana na kuhurumiana kama msingi muhimu wa kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza matendo mema yanayofanywa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na Kwaresima, akieleza kuwa vipindi hivyo ni maalum kwa waumini kumuomba Mungu, kusaidiana na kuonyesha huruma kwa wahitaji katika jamii.

Hafla hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida na kukutanisha viongozi wa Chama na Serikali kutoka wilaya zote za mkoa huo pamoja na viongozi wa dini mbalimbali.
Discussion
Reader comments
0 contributions