Skip to main content

RC DENDEGO AONGOZA KAMATI UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

RC DENDEGO AONGOZA KAMATI UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

RC DENDEGO AONGOZA KAMATI UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO SINGID...

0:00 --:--

Na Saulo Stephen - Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, pamoja na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Singida wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yenye Jumla ya thamani ya Tsh bilioni 3.47, ikihusisha sekta za vijana, elimu, maji, afya, TARURA, mapato ya ndani pamoja na sekta binafsi.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa vijana wa usafirishaji wa Mkombozi Transporter Ltd Makiungu, Daraja la Kimbwi, madarasa manne ya Shule yaIki Sekondari Dadu, Kiwanda cha Mbegu cha Meru-Agro, Mradi wa Maji Mbwanjiki, programu ya uzinduzi wa matumizi ya nishati safi pamoja na ugawaji wa Bima ya Afya kwa Wote katika Shule ya Msingi Ikungi, na ujenzi wa jengo la upasuaji pamoja na wodi ya wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Dendego alisisitiza usafi wa mazingira na matumizi sahihi ya fedha za Serikali ili miradi hiyo iwe na tija kwa wananchi. Pia aliwataka vijana waliopata mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri kurejesha mikopo kwa wakati ili kutoa nafasi kwa wengine kunufaika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, amewataka vijana kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha pamoja na kuwa na mipango mingine ya uwekezaji nje ya miradi waliyoanzisha kwa mikopo ya halmashauri, akieleza kuwa maendeleo yanahitaji uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.