Skip to main content

RC DENDEGO AHIMIZA MAPAMBANO YA RUSHWA KATIKA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Na Saulo Stephen - Singida.

RC DENDEGO AHIMIZA MAPAMBANO YA RUSHWA KATIKA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Na Saulo Stephen - Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amewataka viongozi, watendaji wa serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa, ili fedha za maendeleo ziweze kuwanufaisha wananchi na miradi ya serikali kutekelezwa kwa viwango vinavyotarajiwa.

Dendego ametoa kauli hiyo wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Usimamizi na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Mkoa wa Singida, iliyoandaliwa na TAKUKURU katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Uhasibu (TIA) Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego,

Akizungumza katika warsha hiyo iliyobeba kaulimbiu isemayo "Kuzuia Rushwa ni Jukumu Langu na Lako, Tutimize Wajibu Wetu," Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza TAKUKURU kwa juhudi kubwa inazozifanya katika kuzuia vitendo vya rushwa, hatua ambayo imechangia kuokoa fedha nyingi za umma kabla hazijapotea.

Aidha, amesisitiza kuwa usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo ni nguzo muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo endelevu katika maeneo yao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.