Skip to main content

RC CHALAMILA ASHAURI VYOMBO VYA DOLA KUPEWA KANDARASI YA USAFIRISHAJI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, ameshauri Vyombo vya Dola kupewa kandarasi ya kuingiza mabasi ya mwendokasi, ili yatoe huduma ya kusafirisha abiria kitendo ambacho amesema kitaongeza mshikamano kati yao na Wananchi.

RC CHALAMILA ASHAURI VYOMBO VYA DOLA KUPEWA KANDARASI YA USAFIRISHAJI
Studio Narration JAMBO FM

RC CHALAMILA ASHAURI VYOMBO VYA DOLA KUPEWA KANDARASI YA USA...

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, ameshauri Vyombo vya Dola kupewa kandarasi ya kuingiza mabasi ya mwendokasi, ili yatoe huduma ya kusafirisha abiria kitendo ambacho amesema kitaongeza mshikamano kati yao na Wananchi.

Chalamila amesema hayo hii leo Mei 9, 2026 mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi Namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Konzi Namba 48 kwa Mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania.

Amesema, “leo hii barabara iliyotoka Ikulu inakuja huku Mh. Rais umeijenga kwa zaidi ya bilioni 231 na barabara hii muda sio mrefu itapata mabasi ya mwendokasi, leo nina proposal kwasababu hapa Wakuu wa Vyombo vya Dola wapo,"

"Barabara zote zimepata watoaji huduma pengine kwa barabara hii tungejaribisha Vyombo vya Dola, Polisi, Jeshi na wao waingize mabasi katika barabara za mwendokasi, hii itavutia ule umoja na mshikamano kati ya Vyombo vya Dola na Wananchi kutoogopana zaidi ya kuheshimiana,” aliongeza Chalamila.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.