Ni miaka miwili na wiki tatu madarakani, ambapo Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameamua kumfuta kazi swahiba wake Waziri Mkuu, Ousmane Sonko na kuvunja baraza la Mawaziri la lenye watu 35.
Ikumbukwe kuwa Waziri Mkuu Sonko (52), ndiye kwa hakika alimpa Diomaye "nambari" za kushinda uchaguzi wa Machi 24, 2024 akiwa mgombea maarufu zaidi kabla ya uchaguzi, kama kiongozi wa PASTEF, chama tawala ambacho alikianzisha mwaka 2014.

Diomaye Faye (46), yeye alikuwa ni Katibu Mkuu wa chama hadi siku alipoapishwa kuwa Rais Aprili 2, 2024, ambapo wawili hao walipigana dhidi ya utawala wa Rais wa zamani wa Taifa hilo, Macky Sall ambaye mihula yake miwili ilikuwa inaisha mwaka huo.
Sonko alizuiwa kugombea urais, kutokana na kukutwa na hatia katika kesi ya kudhalilisha jina. Aliamua kuunga mkono SG yake kwa kiti na akashinda kwa kishindo, huku PASTEF pia ikipata wingi wa viti Bungeni.

Katika muda usiopungua mwaka mmoja, Rais huyo na Waziri wake Mkuu walikuwa tayari wanapishana kauli, ikiarifiwa kuwa Sonko ambaye bado anafurahia ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana, anahisi anastahili kushiriki zaidi ikiwa si kiti cha juu.
Hata hivyo, amehoji mamlaka ya Diamaye kutawala nchi hiyo na sasa Rais ameona inatosha na kumfukuza kazi, huku Sonko akisema sasa anaenda kulala akiwa mtu mwepesi.

Hiyo ni kauli ya inayotafsiriwa kuwa Sonko anamaanisha "sasa ngoja uone nitakachofanya" ingawa Diomaye naye ni wa moto, kwani anaweza kumtupa tena gerezani.
Kumbuka, uchaguzi ujao wa Senegal utakuwa Machi 2029, hali itakuwaje? Hili ni la kusubiri na wakati utaongea.
Discussion
Reader comments
0 contributions