Skip to main content

RAIS WA MAHAKAMA YA ICC AWEKEWA VIKWAZO MAREKANI

Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Tomoko Akane na Wakili Mwandamizi wa Taasisi hiyo, Abdoulaye Seye, katika hatua mpya ya kuongeza shinikizo dhidi ya mahakama hiyo.

RAIS WA MAHAKAMA YA ICC AWEKEWA  VIKWAZO MAREKANI

Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Tomoko Akane na Wakili Mwandamizi wa Taasisi hiyo, Abdoulaye Seye, katika hatua mpya ya kuongeza shinikizo dhidi ya mahakama hiyo.

Uamuzi huo umetangazwa jana Jumanne Agosti 18,2026 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio akisema maofisa hao waandamizi wamehusika moja kwa moja katika juhudi za ICC kuchunguza, kuwakamata au kuwafungulia mashtaka viongozi wa nchi ambazo hazijakubali mamlaka ya hiyo, ikiwemo Taifa la Marekani.

Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Tomoko Akane.

Vikwazo dhidi ya Akane na Seye vinawazuia kuingia Marekani kufanya shughuli zao za kifedha kupitia mfumo wa nchi, huku mali zao zilizo ndani ya mamlaka ya nchi hiyo zikifungiwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa ICC imevuka mipaka yake na kutishia mamlaka ya nchi hiyo, hasa kupitia uchunguzi unaowahusu maofisa wa taifa hilo na Israel.

Wakili Mwandamizi wa ICC, Abdoulaye Seye.

Marekani si mwanachama wa ICC na haijawahi kuridhia Mkataba wa Roma ulioanzisha mhimili huo, hivyo imekuwa ikipinga mamlaka ya ICC kuwachunguza na kuwafungulia mashtaka raia wake.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.