Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, amemfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Septemba 8, 2026 kufuatia kufiwa na Mume wake.
Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, Septemba 7, 2026.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Afrika CDC), Dkt. Jean Kaseya, naye amemfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Septemba 8, 2026.
Dkt. Kaseya amefika Kizimkazi kumfariji Rais Samia kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.

Discussion
Reader comments
0 contributions