Skip to main content

RAIS SAMIA: TUFANYE KAZI KWA UADILIFU, MATOKEO YAONEKANE KWA WANANCHI

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi anaowateua kubeba dhamana walizopewa na wathibitishe kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kuleta matokeo yanayoonekana kwa wananchi.

Rais Samia ameyasema hayo, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano Julai 1, 2026, alipozungumza baada ya kuwaapisha viongozi kadhaa aliowateua hivi karibuni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Heshima au dhamana mliyopewa leo sio vyeo tu, kwamba mmebeba vyeo, lakini ni dhamana ambayo inatakiwa ikafanyiwe kazi," amesema.

Amesema wateule hao wameapa siku ambayo wanapaswa kuanza kazi kwani ndipo utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unapoanza rasmi.

"Mjue kwamba mnaingia si kwenda kupumzika kwamba nimepata cheo ngoja ni-relax, bali mnaingia kwenye mchakamchaka wa kweli kweli kwa sababu Dira hii lazima tuitekeleze kwa kasi," amesema Rais Samia.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.