Skip to main content

RAIS SAMIA: HUU NI MWELEKEO WA KUJITEGEMEA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema gawio la Sh1.32 trilioni lililotolewa na mashrika na taasisi za umma ni sehemu ya Serikali ya kuongeza mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi wa kugharamia shughuli za maendeleo.

RAIS SAMIA: HUU NI MWELEKEO WA KUJITEGEMEA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema gawio la Sh1.32 trilioni lililotolewa na mashrika na taasisi za umma ni sehemu ya Serikali ya kuongeza mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi wa kugharamia shughuli za maendeleo.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Jumanne Juni 30, 2026 alipohutubia katika hafla ya siku ya Gawio, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amesema gawio ni sehemu ya lengo la kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi katika kugharimia shughuli za maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tunakwenda polepole tulikotoka ni mbali, lakini tunakwenda polepole bajeti ya mwaka pengo la kujitegemea imebaki kidogo sana.Tukikaza buti, tukifanya kazi kwa bidi bajeti za miaka miwili ijayo tutakuwa tumefanya vizuri,” amesema Dkt Samia.

Dkt Samia ameeleza kuimarika ndivyo Serikali inayozidi kuongeza uwezo wa kutekeleza vipaumbele vya maendeleo vya wananchi kwa rasilimali za ndani.

“Tunaelekea kujitegemea wanasema ‘haiwezekani hadi pale inapowezekana? sasa inawezekana tumeona hapa.” Amesema Dkt Samia.

Mkuu huyo wa nchi, amesisitiza kuwa shabaha yake ni kuona suala la kujitegemea linaondoka kuwa dhamira hadi kuanza kutekelezwa rasmi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.