Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewakumbusha Maafisa Tawala na RasilimaliWatu, kutekeleza wajibu wao na kuleta furaha kwa watumishi wa umma, ili kwa upande mwengine nao wapeleke furaha na neema kwa Watanzania .
Ni katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa AICC, Arusha, akiyaeleza hayo kufuatia maamuzi mbalimbali yanayofanywa na Serikali, katika kuhakikisha maslahi ya Watumishi wa umma nchini yanaboreshwa.
Hatua hiyo inakuja kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa Serikali, kupandisha madaraja watumishi 219,042 ni hatua ya kihistoria katika kuimarisha utumishi wa umma nchini Tanzania.

Hata hivyo, amesema hatua hiyo imepata ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma (2025): +35.1% na ongezeko la kima cha chini sekta binafsi (2025/26): +33.4% .
"Sekta mbalimbali zinakwenda athiriwa na maboresho haya ikiwemo afya, elimu, kilimo, mawasiliano, usafirishaji, nishati, viwanda, biashara, hoteli, michezo, uvuvi, baharini, madini ,utamaduni n.k" alisema Kikwete.
Kwa matokeo hayo, kitakwimu yanaonyesha kasi ya mageuzi ya kiutumishi chini ya Serikali ambayo inaonesha uongozi wa kimkakati unaoweka mbele ustawi wa watumishi na ufanisi wa taasisi za umma.
Discussion
Reader comments
0 contributions