Skip to main content

RAIS SAMIA AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazofanya ikiwemo kuitangaza Tanzania Kimataifa na kukuza mahusiano na Mataifa mbalimbali.

RAIS SAMIA AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA
Studio Narration JAMBO FM

RAIS SAMIA AITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

0:00 --:--

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalla Hamid amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi anazofanya ikiwemo kuitangaza Tanzania Kimataifa na kukuza mahusiano na Mataifa mbalimbali.

Ameyasema hayo Septemba 24, 2026, wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya wakazi wa Singida katika Kikao cha Majadiliano na Mahusiano kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maji mjini Singida.

Amesema juhudi za Rais Samia katika kuitangaza Tanzania na kukuza mahusiano zimeiwezesha nchi kutambulika Kimataifa na kuwa miongoni mwa nchi chache za Afrika zinazopata heshima katika Medani ya Kimataifa.

Ameeleza kuwa Rais Samia pia amekuwa akikuza mahusiano, kutunza amani na upendo, huku akihakikisha anagusa Mtanzania mmoja mmoja kupitia shughuli na mipango mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, Rabia ametambua mchango wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, akisema imekuwa sehemu ya kuwapa Watanzania tabasamu na kuwawezesha kuwa na shughuli za kujipatia kipato.

Amesema mikopo hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia mitaji wanayoipata.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata amepongeza ziara ya Rabia ya kukutana na makundi mbalimbali ya wana-Singida, akiitaja kuwa ni somo zuri na ubunifu mkubwa wa kujenga mahusiano kutoka kwa kiongozi huyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.