Skip to main content

RAIS RUTO: DKT. SAMIA AMEONESHA UONGOZI, TUNAMUUNGA MKONO

Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto amempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuonyesha uongozi kipindi cha kuzivuka changamoto zilizotokea Oktoba 29, mwaka jana.

RAIS RUTO: DKT. SAMIA AMEONESHA UONGOZI, TUNAMUUNGA MKONO
Studio Narration JAMBO FM

RAIS RUTO: DKT. SAMIA AMEONESHA UONGOZI, TUNAMUUNGA MKONO

0:00 --:--

Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto amempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuonyesha uongozi kipindi cha kuzivuka changamoto zilizotokea Oktoba 29, mwaka jana.

Ruto, ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 4, 2026 baada ya kikao cha uwili na Dkt Samia Ikulu jijini Dar es Salaam. Ruto yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto.

Katika maelezo yake, Ruto amemsifu Dkt Samia, akisema ameonyesha uongozi kwa kuunda tume ya kuchunguza mambo hayo na hilo limedhihirisha kuwa, mataifa ya Afrika Mashariki yanaweza kutatua changamoto zake ndani ya mipaka yake.

“Kwa niaba wa Afrika Mashariki, tunakupongeza kwa kuonyesha uongozi kwa Tanzania na ukanda wetu na kuhakikisha kwamba tunaweza kutatua matatizo yetu ndani ya mipaka yetu,” amesema.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.