Skip to main content

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Samoei Ruto, amewasili nchini leo, Mei 4, 2026, kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Studio Narration JAMBO FM

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

0:00 --:--

Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Samoei Ruto, amewasili nchini leo, Mei 4, 2026, kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Akiwa nchini, Rais Ruto atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na mwenyeji wake, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kabla ya viongozi hao kuongoza mazungumzo rasmi ya pamoja kati ya ujumbe wa Tanzania na Kenya, na kuzungumza na waandishi wa habari.

Mazungumzo hayo yataangazia jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kindugu na
kimkakati kati ya Tanzania na Kenya katika biashara, uwekezaji, miundombinu, usafirishaji
na maeneo mengine ya maslahi ya pamoja.

Viongozi hao pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini wa Hati za Makubaliano na Mikataba ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, pamoja na kushiriki Jukwaa la Biashara litakalowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi zote mbili.

Aidha, siku ya Jumanne, Mei 5, 2026, Rais Ruto anatarajiwa kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake kabla ya kurejea nchini Kenya baada ya kuhitimisha ziara yake.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.