Skip to main content

PROF. MKENDA AWAPA NENO WATAFITI WENYE MACHAPISHO MAJARIDA YA KIMATAIFA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

PROF. MKENDA AWAPA NENO WATAFITI WENYE MACHAPISHO MAJARIDA YA KIMATAIFA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda amewahimiza watafiti wenye machapisho katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa kuwasilisha kazi zao, ili kupata fursa ya kutambuliwa kwa mchango wao katika kukuza maarifa, uvumbuzi na maendeleo ya taifa.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Juni 18,2026 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kufunguliwa kwa dirisha la maombi ya Tuzo za nne za Utafiti kwa Watafiti Waliochapisha Matokeo ya Tafiti zao kwenye Majarida yenye Hadhi ya Juu Kimataifa.

Dirisha hilo litakuwa wazi kuanzia Juni 19 hadi Oktoba 31, 2026 na litatoa fursa kwa watafiti wenye sifa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya kutambuliwa na kupewa tuzo.

"Tuzo hizo zitahusisha nyanja nne muhimu za utafiti ambazo ni Sayansi Asilia na Hisabati, Afya na Sayansi Shirikishi, Sayansi za Wanyama na Kilimo, pamoja na Uhandisi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,"amesema. 

Aidha, ameongeza kuwa lengo la tuzo hizo ni kuhamasisha watafiti nchini kufanya tafiti zenye ubora wa hali ya juu, kuongeza idadi ya machapisho ya kisayansi yanayotambulika kimataifa, na kuimarisha mchango wa tafiti katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania.

 “Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watafiti na wabunifu ili kuhakikisha matokeo ya tafiti yanatumika kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo na kuongeza ushindani wa taifa katika nyanja za sayansi, teknolojia na ubunifu,"ameongeza.

Amesema juhudi hizo zinaendana na azma ya Serikali ya kujenga uchumi unaotegemea maarifa, utafiti na matumizi ya teknolojia katika kuongeza tija kwenye sekta mbalimbali za uzalishaji na utoaji huduma.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.