Skip to main content

PROF. KABUDI: MJI WA SERIKALI MTUMBA NI ALAMA YA UWAJIBIKAJI, UTENDAJI BORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema Mji wa Serikali wa Mtumba uliopo mkoani Dodoma ni zaidi ya majengo ya Serikali, na ni alama ya utendaji inayopaswa kuakisi nidhamu, uwajibikaji na bidii kwa watumishi wa umma.

PROF. KABUDI: MJI WA SERIKALI MTUMBA NI ALAMA YA UWAJIBIKAJI, UTENDAJI BORA
Studio Narration JAMBO FM

PROF. KABUDI: MJI WA SERIKALI MTUMBA NI ALAMA YA UWAJIBIKAJI...

0:00 --:--

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema Mji wa Serikali wa Mtumba uliopo mkoani Dodoma ni zaidi ya majengo ya Serikali, na ni alama ya utendaji inayopaswa kuakisi nidhamu, uwajibikaji na bidii kwa watumishi wa umma.

Profesa Kabudi ameyasema hayo leo Oktoba 27, 2026, jijini Dodoma wakati akizungumi na vyombo vya habari kuelekea uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi za wizara, taasisi za Serikali na barabara za lami katika Mji wa Serikali wa Mtumba, utakaofanyika Oktoba 30, 2026.

"Kukua kwa Mji wa Serikali kumeongeza mahitaji ya huduma mbalimbali, zikiwemo usafirishaji, malazi, biashara na huduma nyingine, hali inatoa fursa kwa sekta binafsi kuwekeza na kunufaika na maendeleo ya jiji hili la Dodoma,"amesema.

Aidha, Prof. Kabudi amesisitiza umuhimu wa watumishi wa Serikali kuzingatia nidhamu na kutekeleza majukumu yao kwa juhudi ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Pia, ametoa wito kwa wawekezaji na wafanyabiashara kuchangamkia fursa hizo, hususani kutokana na matarajio ya kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, ambao unatarajiwa kuongeza idadi ya watu wanaosafiri kwenda Dodoma na kuchochea shughuli za kiuchumi.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili wanufaike na maendeleo ya Mji wa Serikali na Makao Makuu kwa ujumla,” amesema.

Katika hatua nyingine, amewataka watumishi wa umma wanaofanya kazi katika Mji wa Serikali kutumia ipasavyo miundombinu iliyowekwa kwa kuongeza uwajibikaji, uadilifu, ubunifu na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Majengo mazuri pekee hayatoshi. Tunahitaji utendaji bora, nidhamu ya kazi na uzalendo ili wananchi waone matokeo ya uwekezaji huu,” amesisitiza.

Amefafanua kuwa uzinduzi wa Oktoba 30 hautakuwa tukio la Serikali kuhamia Dodoma, kwa kuwa hatua hiyo ilishatekelezwa, bali ni uzinduzi rasmi wa miundombinu ya awamu ya kwanza ya Mji wa Serikali.

Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, miundombinu hiyo imeandaliwa kukidhi mahitaji ya utoaji huduma kwa kipindi cha miaka 10 hadi 15 ijayo.

Ameongeza kuwa miundombinu inayohusishwa na maendeleo ya Makao Makuu ya nchi inajumuisha pia Makao Makuu ya Jeshi yaliyopo Kikombo pamoja na miundombinu ya maji na majitaka iliyokamilika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.