Na Tryphone Odace - Kigoma.
Wafanyabiashara na wananchi Mkoani Kigoma, wametakiwa kutumia fursa ya huduma ya EMS ya Posta Tanzania kusafirisha mizigo na bidhaa kwenda mataifa mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani, ili kukuza biashara na kuongeza kipato.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni zinazoendelea kuhamasisha matumizi ya huduma hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Shrika la Posta Tanzania Ferdnand Kabyemela amesema EMS imefanyiwa maboresho na sasa inatoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Amesema huduma hiyo ni rafiki kwa wafanyabiashara, hususan wanaosafirisha bidhaa zinazotokana na shughuli za uvuvi, ikiwemo samaki na dagaa, ambazo ni miongoni mwa bidhaa zinazozalishwa kwa wingi katika Mkoa wa Kigoma.
“Samaki na dagaa ni mazao ambayo yamekuwa na soko kubwa nje ya nchi kwahiyo kwa wafanyabiashara wa kigoma hii fursa kubwa kwani itawarahisishia kufikisha bidhaa zao mataifa mengine,” amesema Ferdnand.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Posta Tanzania, Arubee Ngaruka, amesema wameamua kuimarisha matumizi ya EMS kwa kuwa ni mfumo wa kisasa unaolenga kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwa wananchi.
Discussion
Reader comments
0 contributions