Ushirikiano kati ya shirika la posta Tanzania na zaidi ya nchi 200 duniani umetajwa kuliwezesha shirika hilo kurahisisha huduma kwa wananchi wakati wa kutuma mizigo na kuondoa usumbufu kwa wananchi wanapotuma mizigo hiyo kwenda nchi mbalimbali ikiwemo Marekani.
Hayo yalisemwa na Meneja wa shirika la posta Kigoma Ndagije Chobaliko wakati wa maadhimisho ya siku ya Posta duniani ambapo amesema shirika hilo litaendelea kuwahudumia wananchi na mashirika mbalimbali.
Aidha Chobaliko ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kuendelea kuliamini shirika hilo na kulitumia katika kutuma mizigo kwenda sehemu mbalimbali

Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye picha na viongozi wa posta mara baada ya maadhimisho ya siku posta duniani, Picha na Tryphone Odace
Baadhi ya wakuu wa taasisi ambao wameshiriki maadhimisho hayo walisema shirika la posta limekuwa ni kimbilio la watu wengi pindi wanapotaka kusafirisha mizigo yao na masuala mengine ya kijamii, huku wakiomba watumishi wa shirika hilo kuendelea kujituma ili kuwahudumia wananchi
Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara na wadau ambao wamekuwa wakifanya kazi na shirika hilo walisisitiza umoja kati ya wananchi na shirika hilo uendelee kuwepo kwani shirika la posta Tanzania limeaminiwa na Serikali ili liweze kuwatumikia wananchi kwa kutuma migozo yao bila usumbufu.

Viongozi wa posta na wengine kutoka taasisi za umma na serikali wakikata keki wakati wa maadhimisho ya siku ya posta, Picha na Tryphone Odace
Maadhimisho ya siku ya posta duniani kwa mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo ‘mtandao mmoja wa posta fursa zisizo na mwisho’.
Discussion
Reader comments
0 contributions