Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema halitavumilia watu wanaodaiwa kuhamasishana kufanya vurugu na vitendo vya kihalifu siku ya Novemba 6, 2026 wakati wa hukumu ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP Jummane Muliro imeeleza kuwa wamepokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Watu ndani na nje ya Dar es salaam, wenye nia ya kufanya vurugu hizo.


Discussion
Reader comments
0 contributions