Skip to main content

POLISI WATHIBITISHA KUMSHIKILIA WAKILI PETER MADELEKA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Wakili wa Kujitegemea, Peter Madeleka kwa tuhuma za kudharau amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

​Taarifa iliyotolewa hii leo Agosti 14, 2026 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, imeeleza kuwa Madeleka alikamatwa majira ya saa 9:30 alasiri katika eneo la Mikocheni B, Wilaya ya Kinondoni.

Wakili Peter Madeleka.

​Inaarifiwa kuwa Madeleka anatuhumiwa kukiuka na kudharau amri halali za mahakama hiyo (Mahakama ya Mafisadi), zilizotolewa Julai 27, 2026 na Agosti 13, 2026.

​Kukamatwa kwa Madeleka kunakuja saa chache baada ya kutoa kauli kali dhidi ya taarifa ya Msajili wa Mahakama Kuu iliyowataka mawakili kutokuzungumza na Vyombo vya Habari katika viunga vya Mahakama.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.