Skip to main content

POLISI WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI, KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA MANISPAA SHINYANGA

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

POLISI WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI, KUCHANGIA DAMU  HOSPITALI YA MANISPAA SHINYANGA

Na Eunice Kanumba - Shinyanga.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeshiriki shughuli ya jamii kwa kufanya usafi wa mazingira na kuchangia damu salama katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Zoezi hilo, limeusisha Askari wa vyeo mbalimbali, waliofanya usafi katika maeneo tofauti ya hospitali hiyo kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya na kuchangia damu salama kwa hiari, ili kuokoa maisha ya wahitaji wa huduma hiyo muhimu.

Akizungumza baada ta zoezi hilo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Fraterine Tesha amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kutekeleza wajibu wake si tu katika kulinda usalama wa raia na mali zao, bali pia kushiriki shughuli za kijamii zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Aidha, ameushukuru uongozi wa Hospitali hiyo kwa ushirikiano na kutoa wito kwa taasisi na makundi mengine kujitokeza kuchangia damu salama, ili kuokoa maisha ya wahitaji hasa akina mama wajawazito na wale waliopata ajali.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuona umuhimu wa kuchangia damu salama, pamoja na kushiriki kuboresha mazingira ya Hospitali.

Kufuatia tukio hilo, Jambo Media imezungumza na baadhi ya wananchi akiwemo Stephano Kabalo na Makanyanga Peter, kuhusu Jeshi la polisi kujitoa kwa jamii ambapi wamesema ni jambo jema kuwa karibu na jamii na kufanya matendo ya huruma hususan uchangiaji wa damu.

Wamesema, uchangiaji wa damu ni muhimu katika kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma za dharura za afya, wakiwemo waathirika wa ajali, wanawake wanaopoteza damu wakati wa kujifungua, wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji nk.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.