Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetolea ufafanuzi tukio la mauaji ya watu wanne na majeruhi mmoja lililotokea katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo Kiwangwa wilayani Bagamoyo.
Tukio hilo, linadaiwa kutokea Machi 12, 2026 majira ya saa 20.45 usiku, katika maeneo ya Kidudumale Mwetemo, baada ya Boniphace Ikilala Ndalemi (53), kuwakata kwa panga watu watano.
Inaarifiwa kuwa, Mtuhumiwa alifika kilabuni na kuagiza pombe ya kienyeji aina ya Mabuya akanywa na kuondoka na ilipofika majira ya saa 2:15 usiku alirudi tena kilabuni akimdai mmiliki wa kilabu hicho, Asha Khamis Athuman shilingi 5,000 ambayo alidai aliiacha alipofika kilabuni hapo.

Mtuhumiwa alianza kuzozana na mmiliki wa kilabu hicho cha pombe kuhusu pesa hiyo na baadhi ya watu waliokuwa eneo hilo walikua wakimsaidia Asha Khamis kuwa Boniphace Ndalemi hakuacha pesa ya ziada na ndipo alianza kuwashambulia kwa panga.
Taarifa za tukio hilo zilifika Jeshi la Polisi na walifika eneo la tukio ambapo mtuhumiwa alikaidi amri za Polisi, hali iliyosababisha askari kumpiga risasi mguuni na alifariki akiwa njiani akipelekwa kwenye Matibabu.
Discussion
Reader comments
0 contributions