Skip to main content

POLISI WAFAFANUA TUKIO LA WIZI WA JENEZA HAI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limefafanuzi tukio la kuibiwa kwa jeneza lililotokea katika Kijiji cha Mbweera, Kata ya Masama, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, jirani na Kanisa la KKKT Ushirika wa Masama Kati.

POLISI WAFAFANUA TUKIO LA WIZI WA JENEZA HAI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limefafanuzi tukio la kuibiwa kwa jeneza lililotokea katika Kijiji cha Mbweera, Kata ya Masama, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, jirani na Kanisa la KKKT Ushirika wa Masama Kati.

Taarifa ya Polisi inaeleza kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa Agosti 31, 2026, ambapo Ombeni Elifura Ndosa aligundua kuwa jeneza lililokuwa katika ofisi yake ya biashara lilichukuliwa na watu ambao hadi sasa hawajatambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopokelewa, watu hao waliingia katika eneo hilo na kufanikiwa kuchukua jeneza hilo na kulitelekeza kwenye njia ya kuingilia Kanisani, baada ya kuona mwanga wa tochi ukiwaelekea wakati wa usiku.

Katika tukio hilo, hakuna kitu kingine kilichoibwa na wala mtu aliyepata madhara ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa wahusika walitumia njia ya kufungua mlango na kubeba jeneza hilo.

Aidha, ndugu Ombeni Elifura Ndosa ameeleza kuwa alikuwa na utaratibu wa kufunga mlango kwa kuegesha bila kutumia kufuli, akiamini kuwa hakuna mtu angeweza kuiba jeneza.

Uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini wahusika wa tukio hilo, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria kwa hatua stahiki.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.