Skip to main content

POLISI WAENDESHA MSAKO MADEREVA WANAOVUNJA SHERIA KAHAMA

Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, limewataka waendesha pikipiki wa magurudumu matatu (bajaji) na maguta, kuzingatia sheria za usalama barabara ikiwa ni pamoja na kuacha kupakia mizigo mingi kupita kiasi, hali inayosababisha kushindwa kuona upande wa kulia na kushoto na upande wa nyuma.

POLISI  WAENDESHA MSAKO MADEREVA WANAOVUNJA SHERIA KAHAMA
Studio Narration JAMBO FM

POLISI WAENDESHA MSAKO MADEREVA WANAOVUNJA SHERIA KAHAMA

0:00 --:--

Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga, limewataka waendesha pikipiki wa magurudumu matatu (bajaji) na maguta, kuzingatia sheria za usalama barabara ikiwa ni pamoja na kuacha kupakia mizigo mingi kupita kiasi, hali inayosababisha kushindwa kuona upande wa kulia na kushoto na upande wa nyuma.

Rai hiyo, imetolewa na Mrakibu Msaidizi (SP) Frola Nangawe ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Manispaa ya Kahama, wakati wa msako wa wavunjifu wa sheria za usalama barabarani uliombatana na utoaji wa elimu kwa madereva hao, uliofanyika eneo la Lumambo njia panda ya Kwenda Halmashauri ya Ushetu na barabara ya maziwa makuu.

Nangawe amesema, madereva wengi wanakiuka sheria za usalama barabarani licha ya kuwa wanapewa elimu za mara kwa mara katika vijiwe vyao, kuhusu usalama wao na vyombo vyao wanapokuwa Barabarani.

“Leo tuko hapa tumeamua kufanya msako kwa madereva wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani,tumeendelea kuwapa elimu na wengine tumewachakulia hatua kwa kushusha mizigo mikubwa waliopakia kwenye Babaji zao,yani mzigo wa kupakia kwenye fuso watu wanapakia kwenye bajaji,hawaoni kushoto wala kulia hii hatari kwa usalama wao na watumiaji wengine wa barabara. ” Amesema Nangawe.

Nangawe pia amewataka madereva kukata bima ya vyombo vyao vya moto, kwani ni takwa la kisheria ili ziwasaidie pindi wanapopata au wanaposababisha ajali barabarani.

“Niwaombe mkate bima za vyombo vyenu,hii itawasaidia sana pindi mtapopata ajali maana tunajua hali zetu za vipato,sasa bima ni takwa la kisheria niwaombe mkate bima maana unaweza kuwa upo makini lakini ukasababishiwa ajali na mtu mwingine au wewe ukasababisha ajali na bima ikakusaidia,” ameongeza Nangawe.

Nao badhi ya wananchi wa manispaa ya Kahama, wamelipongeza jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuendesha zoezi hilo na kuwaomba wazidi kuendelea kutoa elimu na kuwachukulia hatua wote wanaokiuka sheria.

“Tunapongeza sana zoezi hili linaliondelea kufanyika hapa mataa,kwakweli madereva wanaendesha rafu sana licha ya kuwa tumeekewa taa lakini bado watu hawaheshimu taa wanapita tu kwa kasi kila wakati,niwaombe polisi wasiishie leo waendelee na maeneo mengine ili kuhakikisha tunatomeza ajali katika mji wetu,” Walisema kwa nyakati tofsuti mzee Said Rajabu na Anna Abdalah.

Baadhi ya madereva pikipiki ambao walikamatwa katika oparesheni hiyo, walikiri makosa wakisema wataenda kuwa mabalozi kwa madereva wengine,

“Mimi sioni kama nimeonewa ni kweli hapa nimekosea mana mbao nilizobeba ni nyingi na sijavaa kofia ngumu sasa hapo kosa ni lanani kama siyo mimi,ila sasa nitaenda kuwa balozi kwa wenzangu wote kuhusu mambo yakutofanya tuwapo barabarani,” Amesema Boaz Hashimu.

Katika zoezi hilo, baadhi ya madereva waliokamatwa walitozwa faini kwa makosa mabalimbali,huku wengine wakipewa onyo kwa matukio waliofanya na wengine vyombo vyao kuchuliwa na kupelekwa kituoni kwa ajili ya kukosa faini na wengine kuwa na makosa makubwa na ubovu wa vyombo vyao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.