Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesemq linaendelea na uchunguzi wa mauaji ya Leah Mazengo (50), mkazi wa Kijiji cha Lamaiti, kilichopo Wilayani Bahi, ambaye alikutwa amefariki shambani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Gallus Hyera, amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu Leah aliuawa kwa kukabwa shingo na aliyekuwa mume wake.

Leah aliondoka nyumbani Julai 20, 2026 kuelekea shambani lakini hakurejea ambapo msako wa ndugu na watoto wake ulibaini mwili wake ukiwa umefichwa chini ya magunia ya alizeti yaliyokuwa shambani.
Inadaiwa kuwa kabla ya tukio hilo, marehemu na mume wake walikuwa na migogoro ya kifamilia, huku chanzo cha mauaji hayo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Discussion
Reader comments
0 contributions