Skip to main content

POLISI TUNAWAPENDA NDIO MAANA TUNAWAKAMATA - RPC KATAVI

Na Daniel Gahu - Katavi.

POLISI TUNAWAPENDA NDIO MAANA TUNAWAKAMATA - RPC KATAVI

Na Daniel Gahu - Katavi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, SACP. Kaster Ngonyani kwa kushirikiana na kikosi Maalum cha usalama barabarani kimefanya oparesheni Kali ya kuwakamata waendesha pikipiki (Bodaboda) ambao huendesha pikipiki pasipo kufuata Sheria za barabarani ikiwemo wenye makosa ya kuchomoa site mirror na taa halisi za pikipiki.

Oparesheni hiyo imefanyika katika maeneo ya mji wa Manispaa ya Mpanda kwa lengo la kupunguza na kutokomeza ajali nyingi za barabarani ambazo hutokea kutokana na uzembe wa watumiaji wa barabara na watumiaji wa vyombo vya moto kwa ujumla.

Amesema, "Waendesha pikipiki mnafumua ile mafra, mnapiga kelele, hamtaki kuvaa Helmet, mnabeba mishikaki na mnavunja site Mirror, tumeona wananchi wa Mkoa wa Katavi wanalalamika sana na mnafunga taa zenye Mwanga mkali sana hadi mnapelekea kusababisha ajali Kwa watumiaji wengine wa barabara."

Kutokana na kadhia hiyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa Kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani pamoja na vikosi vingine waliamua kufanya msako wa kuwakamata waendesha pikipiki na pikipiki ambazo hazifuati Sheria za usalama barabarani.

"Naamini mtakapo lipa faini hapa kutokana na makosa yenu, mtakuwa mstari wa mbele katika kuzingatia matumizi sahihi ya vyombo vya moto mkiwa barabarani, na nitoe rai kwa waendesha pikipiki zinazoelekea machimboni wamekuwa wakibebana wengi kupita kiasi, pikipiki moja inabeba watu saba hadi wanakaribia kudondoka," alieleza Kamanda Ngonyani.

Amesema, "nyie bado ni vijana wadogo, familia zinawategemea na Taifa linawategemea sasa mkifa mkiwa bado wadogo itakuwa ni hasara kubwa kwa taifa kwani wazazi wenu wanahitaji misaada kutoka kwenu."

Amesema, Jeshi la Polisi tunawapenda sana na ndio maana tunawakamata ili mbadilike, hatutaki kusikia taarifa za vifo kuwahusu nyie Bodaboda kwani mmekuwa wahanga wakubwa wa ajali za barabarani kwasababu ya kutokutii sheria za matumizi sahihi ya barabara.

Aidha, Kamanda Ngonyani ametoa wito kwa waendesha vyombo vya moto kuendesha vyombo vyao kwa kuzingatia Sheria za barabarani huku akisema kuwa Jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria wale wote watakaobainika na makosa ya matumizi ya vyombo vyao wakati wakiwa barabarani.

"Niwaombe sana, madereva Bodaboda, Bajaj, Daladala na Mabasi ya masafa marefu kuzingatia sheria na taratibu zote za barabara ili kutokomeza ajali ndani ya Mkoa wa Katavi, Katavi bila ajali inawezekana," alisema RPC.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.