Skip to main content

POLISI TABORA WATAKIWA KUHUDUMIA WANANCHI KWA NIDHAMU, UADILIFU

Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama amewaagiza Askari Polisi Mkoa wa Tabora kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia nidhamu, weledi na uadilifu wakati wa kutekeleza majukumu yao ya ulinzi na usalama.

CP Mkama ametoa agizo hilo akiwa katika ziara yake wilayani Nzega na Igunga ambapo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua vitendo vya uhalifu.

Aidha, amewataka Polisi Kata kuongeza juhudi za kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kutoa elimu kuhusu madhara ya vitendo vya uhalifu hususan mauaji yanayotokana na migogoro ya kifamilia na ndoa. 

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Constantine Mbogambi amesema ushirikiano kutoka kwa wananchi umeendelea kuwa chachu ya mafanikio katika kudhibiti vitendo vya uhalifu mkoani humo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.