Skip to main content

POLISI SINGIDA YADHAMIRIA KUIMARISHA UHUSIANO WAKE NA JAMII

Na Saulo Stephen - Singida.

POLISI SINGIDA YADHAMIRIA KUIMARISHA UHUSIANO WAKE NA JAMII

Na Saulo Stephen - Singida.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limeendelea kuonyesha mwelekeo mpya wa utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuimarisha uhusiano wake na jamii kupitia matendo ya kijamii yanayolenga kujenga upendo, mshikamano na ushirikiano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amon Kakwale, amesema askari wa jeshi hilo wametembelea Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Sabasaba, ambapo walijumuika na wanafunzi wenye ulemavu kwa kushiriki chakula pamoja kama ishara ya upendo, kujali na kuendeleza ukaribu kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Amon Kakwale.

Kamanda Kakwale amesema Jeshi la Polisi linaendelea kujibadilisha na kuwa la kisasa, linaloweka mbele ushirikiano na wananchi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.

Amebainisha kuwa pamoja na kutekeleza majukumu yake ya msingi, jeshi hilo linaendelea kuendesha programu za Polisi Jamii, kutoa elimu kwa wananchi na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ili kuongeza imani ya wananchi na kuimarisha usalama."Usalama ni jukumu la kila mmoja wetu.

Tukishirikiana kama jamii, tunajenga mazingira salama, yenye amani na mshikamano," amesema Kamanda Kakwale.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.