Skip to main content

POLISI MWANZA WACHUNGUZA USAMBAZWAJI WA VIPEPERUSHU VYA UCHOCHEZI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeanza uchunguzi wa kina kuhusiana na uwepo wa vipeperushi vinavyosambazwa barabarani, vyenye maudhui ya uchochezi wa vurugu na uvunjifu wa amani.

POLISI MWANZA WACHUNGUZA USAMBAZWAJI WA   VIPEPERUSHU VYA UCHOCHEZI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeanza uchunguzi wa kina kuhusiana na uwepo wa vipeperushi vinavyosambazwa barabarani, vyenye maudhui ya uchochezi wa vurugu na uvunjifu wa amani.

Katika taarifa yake, Kamanda w Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilboard Mtafungwa  amesema vipeperushi hivyo vilianza kusambazwa kuanzia Juni 5 - 6, Juni 2026 katika maeneo ya Mtaa wa Libert, Jijini Mwanza, pamoja na eneo la Kanyama–Kisesa, Wilaya ya Magu.

Amesema, “Vipeperushi hivyo vinasambazwa na watu ambao bado hawajatambuliwa na uchunguzi unaendelea, ili kubaini wahusika.”

Aidha, Polisi imeonya kuwa haitaruhusu mtu yeyote au kikundi chochote kuhamasisha vitendo vya vurugu au uvunjifu wa amani nchini.

“Kwa hali hiyo, tunawaomba wakazi wa Mkoa wa Mwanza kutoa taarifa kwa kituo cha Polisi kilicho karibu au mamlaka nyingine za Serikali endapo watawatambua watu wanaohamasisha vitendo hivyo, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa,” alisema Mutafungwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.