Skip to main content

POLISI KUENDELEZA UKAGUZI MABASI YANAYOFANYA SAFARI ZA USIKU

Na William Bundala - Kahama.

POLISI KUENDELEZA  UKAGUZI MABASI YANAYOFANYA SAFARI ZA USIKU

Na William Bundala - Kahama.

Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani nchini limesema kuwa litaendelea na ukaguzi wa mabasi yanayofana safari za usiku kwa lengo la kuimarisha usalama barabarani na kuhakikisha sheria za usafirishaji zinazingatiwa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Mwakabonga wakati wa zoezi la kukagua mabasi hayo lililofanyika katika kata ya Kagongwa manispaa ya Kahama mkoani Shiyanga.

Mwakabonga amesema zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Jeshi la Polisi za kuzuia ajali za barabarani ambazo mara nyingi husababishwa na uzembe wa madereva, uchovu na ukiukwaji wa sheria za usalama.

“Ukaguzi huu ni juhudi za jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha tunapunguza kama si kumaliza kabisa ajali za barabarani zinazotokana na uzembe wa madereva,Uchovu unaosababishwa na usingizi na wengine kutofuata sheria za usalama baraarani” Amesema Mwakabonga.

Ameongeza kuwa katika zoezi hilo la Ukaguzi wamekagua vitu mbambali ikiwemo  hali ya mabasi, nyaraka za madereva,matumizi ya mikanda, mwendo wa magari na hali ya matairi na amewakumbusha madereva kuepuka mwendo kasi na kuhakikisha wanazingatia muda wa mapumziko ili kupunguza hatari ya ajali.

“Ukaguzi wa leo umelenga kukagua hali ya chombo cha usafiri,nyaraka za madereva Pamoja ukiukkwaji wa sheria za barabarani ikiwemo uvaaji wa mikanda lakini pia tumewakumbusha madereva kuepuka  mwendo kasi na kuhakikisha wanapata mud awa kupumzika ili kuunguza ajali kutokana na uchovu wa safari” Ameongozea Mwakabonga.

Kwa upande wao badhi ya Maderev awa masafa marefu wamesema kuwa ukaguzi huu unawaimarisha katika utendaji wao kwani unawafanya kukumbuka sheria mara kwa mara na kuliomba jeshi la polisi kutoa elimu hii na kwa madereva wa magari madogo ya abiria na binafsi kwani ajali zingine zinasababishwa na wao.

“Ukaguzi huu kwetu sisi madereva unatusaidia sana kwakuwa tunakumbushwa sheria mara kwa mara lakini cha msingi tunaomba watoe elimu kwa madereva wa magari madogo ya abiria na magari binafsi kwa sabababu ajali zingine zinasababishwa na wao” Wamesema Madereva hao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.