Skip to main content

PAMBA JIJI WAPANIA 'KUISULUBU' SIMBA SC

Na Kusaga ungura - Mwanza.

PAMBA JIJI WAPANIA 'KUISULUBU' SIMBA SC

Na Kusaga ungura - Mwanza.

Katika kuelekea mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Simba SC, Msemaji wa Pamba Jiji FC, Moses William amekuja na
kaulimbiu mpya inayosema "Hii ni yetu".

Akiongea na vyombo vya Habari, Moses amebainisha kuwa, lengo la kutumia kaulimbiu hiyo, ni kutaka kutumia dimba lao la nyumbani kwa kushinda mchezo huo.

Amesema, licha ya kupoteza mara kadhaa mbele ya Simba SC, lakini safari hii bechi lao la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Franciss Baraza wameiandaa tumu vizuri ili kufanikisha lengo.

Aidha, Moses ametaja bei za viingilio katika mchezo huo ambapo mzunguko ni 10, 000, VIP 20,000, vvip 30,000 akisema lengo ni kuwapa fursa za mashabiki kutafuta fedha na kuepuka athari za kimtandao wakati wa kukata tiketi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.