Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imebaini mapungufu katika utekelezaji wa mkataba wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es Salaam, kati ya WADATS na Metro Link City Company Limited.
Miongoni mwa mapungufu hayo ni mabadiliko ya muundo wa utekelezaji wa mkataba bila ushahidi wa idhini ya mamlaka husika.

Kingine ni kutokuwepo kwa uthibitisho wa thamani ya mali zilizokabidhiwa pamoja na kutolipwa kwa kodi ya mapato ya dola za Marekani 90,000.
Aidhq, Kamati imeeleza kuwa hali hiyo inazua hoja kuhusu usimamizi wa mkataba, mali za umma na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Discussion
Reader comments
0 contributions