Na Afarah Suleima, Babati - Manyara.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imerejesha zaidi ya shilingi milioni 100 katika kipindi cha Aprili hadi Septemba mwaka huu, kufuatia operesheni maalum iliyofanyika katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Burunge, Wilayani Babati.
Akitoa taarifa ya robo mwaka, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Anthony Gang'olo, amesema katika uchunguzi huo walibaini kuwepo kwa utaratibu usio halali wa kufanya vikao visivyo na uhalali pamoja na kujilipa posho za kila mwezi kinyume na utaratibu wa jumuiya hiyo.

"Katika ufuatiliaji huo, TAKUKURU ilikagua nyaraka na taratibu za malipo kwa kipindi cha mwaka 2024 hadi 2025 na kubaini kuwepo kwa malipo yaliyotokana na posho pamoja na vikao visivyo halali," amesema Gang'olo.
Katika hatua nyingine, Gang'olo amesema TAKUKURU imerejesha zaidi ya shilingi milioni moja za mradi wa ujenzi wa madarasa matatu na vyoo matundu sita katika Shule ya Msingi Namalulu, ya Wilayani Simanjiro.

Discussion
Reader comments
0 contributions