Na Adam Msafiri - Mara.
Matukio ya uhalifu ikiwemo mauaji, uvunjaji na wizi yamepungua kwa kiasi kikubwa mkoani Mara kufuatia oparesheni maalum zinazofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi.
Akizungumza siku za hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo,amesema kuwa jitihada hizo zimeleta mafanikio makubwa katika kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita.

Aidha ameeleza kuwa kwa sasa matukio ya mauaji, uvunjaji na wizi yamepungua kwa kiwango kikubwa, hali inayodhihirisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Jeshi la Polisi na wananchi ambapo naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, ametoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu,akisisitiza kuwa serikali haitawavumilia.

Kanali Mtambi amewataka askari polisi kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia maadili ya kazi yao ili kudumisha amani na usalama wa raia na mali zao.
Baadhi ya wananchi na wakazi wa mkoa wa Mara akiwemo mbunge mstaafu wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo, wamepongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu mkoani humo.
Discussion
Reader comments
0 contributions