Skip to main content

NYUMBA 11 NA KANISA VYAEZULIWA NA MVUA YA UPEPO KASULU

Nyumba 11 ikiwemo Kanisa moja vimeezuliwa na nyingine kubomoka kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika Kitongoji cha Makamba, Kijiji cha Nyamyusi, Kata ya Nyamyusi, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mikoaniKigoma.

NYUMBA 11 NA KANISA VYAEZULIWA NA MVUA YA UPEPO KASULU
Studio Narration JAMBO FM

NYUMBA 11 NA KANISA VYAEZULIWA NA MVUA YA UPEPO KASULU

0:00 --:--

Nyumba 11 ikiwemo Kanisa moja vimeezuliwa na nyingine kubomoka kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika Kitongoji cha Makamba, Kijiji cha Nyamyusi, Kata ya Nyamyusi, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, mikoaniKigoma.

Akizungumza kwa njia ya simu, Diwani wa Kata ya Nyamyusi, Nathanael Njali, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 28, 2026, ambapo tathmini ya awali imebaini kuwa nyumba 11 na kanisa moja zimeezuliwa, huku vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Kisuma vikiathiriwa na mvua hizo.

Amesema wanaendelea kufuatilia na kutathmini madhara zaidi yaliyotokea, huku akieleza kuwa hadi sasa hakuna madhara yaliyoripotiwa kwa binadamu.

Kwa upande wake, mmoja wa wananchi wa Kata ya Nyamyusi, Zakayo Samwel, amesema mvua hiyo iliyoambatana na mawe na upepo mkali ilinyesha kwa takribani nusu saa na kusababisha uharibifu huo.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamyusi, Zakayo Halalawe, amesema viongozi wa kijiji hicho wanaendelea kutembelea kaya zilizoathiriwa ili kubaini ukubwa wa madhara na kuwasilisha taarifa katika Kamati ya Maafa ya Wilaya kwa hatua zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.