Skip to main content

NMB YAKABIDHI VITI, MEZA SHULE MBILI ZA SEKONDARI BUHIGWE

Benki ya NMB imetoa msaada wa samani zenye thamani ya Shilingi 10,220,000 kwa shule ya Sekondari Buhigwe na Shule ya Sekondari Biharu zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

NMB YAKABIDHI VITI, MEZA SHULE MBILI ZA SEKONDARI BUHIGWE
Studio Narration JAMBO FM

NMB YAKABIDHI VITI, MEZA SHULE MBILI ZA SEKONDARI BUHIGWE

0:00 --:--

Benki ya NMB imetoa msaada wa samani zenye thamani ya Shilingi 10,220,000 kwa shule ya Sekondari Buhigwe na Shule ya Sekondari Biharu zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Msaada huo unajumuisha samani za shule zenye jumla ya viti na meza 65, zilizolenga kuimarisha mazingira ya wanafunzi kujifunzia pamoja na kuwawezesha walimu kutekeleza majukumu yao katika mazingira bora zaidi.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Buhigwe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, George Emmanuel Mbilinyi, ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo kwa niaba ya Serikali.

Aidha, ameiomba benki hiyo kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa manufaa ya wananchi, hususan katika sekta ya elimu.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari, Bi. Silvia Ntigiri, ameishukuru NMB kwa mchango huo na kuahidi kuwa samani zilizopokelewa zitatunzwa vizuri na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuhakikisha zinachangia kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Naye Meneja wa NMB Tawi la Buhigwe, Bi. Pendo Waziri, amesema msaada huo ni sehemu ya uwajibikaji wa kijamii wa benki hiyo (CSR), unaolenga kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kuchochea maendeleo ya jamii.

Ameeleza kuwa NMB itaendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe katika nyanja mbalimbali za maendeleo, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya benki hiyo ya kuchangia ustawi wa jamii.

Msaada huo unatarajiwa kuwa na mchango muhimu katika kuboresha mazingira ya shule na kuunga mkono juhudi za kuinua ubora wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.