Skip to main content

NI WAJIBU WETU KUWAHUDUMIA WENYE MAHITAJI MAALUM - DKT. MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kushiriki kugharamia huduma kwa watu wenye ulemavu na watoto walio katika mazingira magumu, akisisitiza kuwa kuwahudumia ni wajibu wa Serikali na jamii.

NI WAJIBU WETU KUWAHUDUMIA WENYE MAHITAJI MAALUM - DKT. MWIGULU
Studio Narration JAMBO FM

NI WAJIBU WETU KUWAHUDUMIA WENYE MAHITAJI MAALUM - DKT. MWIG...

0:00 --:--

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kushiriki kugharamia huduma kwa watu wenye ulemavu na watoto walio katika mazingira magumu, akisisitiza kuwa kuwahudumia ni wajibu wa Serikali na jamii.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo, Jumatatu, Oktoba 5, 2026, alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia maendeleo na maboresho ya vituo vya huduma na diakonia vya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, iliyofanyika katika viwanja vya Tanga Beach Resort, jijini Tanga.

“Majukumu yanayohusu watoto wa Kitanzania walioko katika mazingira magumu, watoto wa Kitanzania wenye mahitaji maalum kama hawa, tuyabebe wenyewe kama Watanzania,” amesema.

Ameeleza kuwa kupungua kwa misaada kutoka kwa wahisani wa nje hakujapunguza mahitaji ya makundi hayo, hivyo Watanzania wanapaswa kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa.

Waziri Mkuu amelipongeza kanisa kwa kutoa huduma za elimu, afya na malezi, akisisitiza kuwa watoto hawapaswi kukosa elimu kutokana na ulemavu wa kuona. Pia, amewataka maafisa maendeleo ya jamii kuendelea kuvitambua vituo vinavyohudumia makundi hayo na watu wanaohudumiwa, pamoja na kuhakikisha vituo hivyo vinasajiliwa rasmi ili kurahisisha uratibu wa misaada.

Katika hatua nyingine, amewataka viongozi wa halmashauri kuwasaidia watu wenye ulemavu wasioweza kujitegemea badala ya kuwapa barua za kuzunguka kuomba michango.

“Nikasema watu hawa wasiandikiwe barua kwenda kuchangisha, badala yake wachangiwe warudi wakaendeshe maisha yao,” amesema.

Ameeleza kuwa wapo watu wenye ulemavu wanaohitaji mikopo ili kuendeleza shughuli za uzalishaji, huku wengine wakihitaji msaada wa maisha ya kila siku. Amesema ameelekeza wasilazimishwe kujiunga na vikundi ili kupata mikopo na kwamba Serikali inaangalia namna ya kuboresha mifumo ya kuwasaidia wasioweza kujitegemea pamoja na wanaowatunza.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.