Skip to main content

NI KISHINDO SINGIDA: WASIRA KUHITIMISHA ZIARA

Na Saulo Stephen – Singida.

NI KISHINDO SINGIDA: WASIRA KUHITIMISHA ZIARA

Na Saulo Stephen – Singida.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Masato Wasira, amepokelewa kwa shamrashamra na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanachama pamoja na wakereketwa wa chama hicho katika Manispaa ya Singida, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Stendi ya Zamani mjini Singida.

Mapokezi hayo yameongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, akishirikiana na viongozi wa chama wa ngazi mbalimbali, huku mamia ya wanachama na wananchi wakijitokeza kumpokea kwa nyimbo, ngoma za asili na bendera za chama.

Ziara ya Wasira iliyoanza Agosti 19, 2026, imepitia wilaya mbalimbali za Mkoa wa Singida, ambapo amefanya mikutano ya ndani na kukutana na viongozi, wanachama na wakereketwa wa CCM, akisisitiza umoja, mshikamano na matumizi ya fursa za maendeleo, hususan katika sekta za kilimo, ufugaji na uchimbaji wa madini.

Mkutano wa hadhara wa leo unahitimisha rasmi ziara hiyo ya siku tatu mkoani Singida.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.