Skip to main content

NHIF:JIUNGENI KWENYE VIKUNDI MKATE BIMA YA UMOJA AFYA KUEPUKA GHARAMA ZA MATIBABU

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujiunga kwenye vikundi ili wakate bima ya umoja afya ili iwasaidie kupunguza gharama za matibu pindi wanapopta matatizo ya kuugua au kuuguliwa.

NHIF:JIUNGENI KWENYE VIKUNDI MKATE BIMA YA UMOJA AFYA KUEPUKA GHARAMA ZA MATIBABU
Studio Narration JAMBO FM

NHIF:JIUNGENI KWENYE VIKUNDI MKATE BIMA YA UMOJA AFYA KUEPUK...

0:00 --:--

Wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kujiunga kwenye vikundi ili wakate bima ya umoja afya ili iwasaidie kupunguza gharama za matibu pindi wanapopta matatizo ya kuugua au kuuguliwa.

Rai hiyo imetolewa na afisa wanachama kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) Peter Hongole wakati akizungumza na Jambo Fm baada ya kumaliza kutoa elimu kwa kikundi cha Mshikamano (KIMSO) kilichopo mtaa wa majengo Kahama ambacho kimejiunga na kifushi cha Umoja afya.

Hongole amesema kuwa kifurushi cha bima ya umoja afya ni kwa ajili ya vikundi na muhimu kikundi kiwe kiwe kimesajiliwa ambacho kila kikundi kinatakiwa kiwe na watu kuanzia kumi na wawe na shughuli inayofahamika katika jamii kama mama lishe,Bodabod ana vingine vinavyofanana na hivyo.“Niwashauri tu wakazi wa Kahama kujiunga na kifurushi hiki cha bima ya umoja afya,Bima hii itawasaidia wanakikundi kupata matibabu kwa gharama nafuu sana,na kikundi kinatakiwa kiwe na watu kuanzia kumi na wawe wanafanya shughuli za kijamii kama mama lishe,bodaboda na nyigine zinazofanana na hizo”Amesema Hongole.

Sambamba na hayo Hongole amesema kuwa bima ya Umoja afya ni rahisi na nafuu kwa kila Mtanzania na kwamba kila mwanachama atachangia kiasi cha shilingi elfu sitini kwa mwaka na unapata huduma kuanzia zahanati hadi katika vituo vya afya na kupata rufaa hadi hospitali za wilaya.

“Bima ya Umoja afya ni rahisi na nafuu sana kwa kila mtanzania,kila mwanachama atachangia kiasi cha shilingi elfu sitini tu kwa mwaka na ataweza kupata huduma kuaniza ngazi ya zahanati na kituo cha afya na bado inawapa mwanya wa kuwaunga wenza wao Pamoja na watoto pia” Ameongezea Hongole.

Kwa upande wake katibu wa kikundi cha Mshikamano (KIMSO) Emmanuel Malya amesema kuwa wameamua kujiunga na huduma hiyo ya Umoja Afyakwasababu familia nyingi hazina uwezo wa kifedha kukabilina na matibu hivyo huduma hiyo itawasaidia kupata huduma kwa wakati na gharama ndigo ambayo kila familia inaweza kuhimili.

“Tuliamua wanachama wote tujiunge katika kifurushi hiki kwasababu hali ya familia zetu tunazijua matibabu bei ghali na hatuna fedha za kuweza kumudu ila kwa mpango huu ni matumaini yangu wananchi wote hasa wanachama wa kikundi cha Mshikamano wataweza kumudu” Alisema Malya.

Kwa upande wao baadhi ya wananchama wa kikundi cha Mshikamo Vicent Nkwabi na wamaesema kuwa wamefurahishwa na huduma hiyo ya bima ya vikundi na kuomba wahusika watoe huduma kulingana na gharama wanazotoa na siyo Kwenda zahanati au kituo cha afa na kukosa huduma.

“Tumefurahi sana kwa kupata maelezo ya kifurushi hiki cha bima,tuwaombe watoa huduma wazidi kusimamia na kuhakikisha tunapata huduma kulingana na fedha tunazotoa na siyo Kwenda mahala unapewa panado huku tunatoa hela” Wamesema wanachama hao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.