Na Saulo Stephen - Singida.
Diwani wa Kata ya Mkwese iliyopo Halmamashauri ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, Shigela Ng'wigulu amezindua kliniki maalumu ya kusikiliza, kupokea na kutatua kero za Wananchi wa Kata hiyo.
Uzinduzi huo, umefanyika katika ofisi ya kata Mkwese ambapo katika zoezi hilo Diwani Shigela kwa kushirikiana na Mtendaji wake wa Kata, Wataalamu na Wenyeviti wa Vitongoji, wamepokea kero mbalimbali za wananchi na kuzishughulikia kwa kushauri huku zingine wakichukua hatua za Moja kwa Moja.

Katika kliniki hiyo wananchi mbalimbali kutoka kata ya Mkwese waliojitokeza na kuwasilisha kero zao ambazo zilitatuliwa na Diwani Shigela kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa wenyeviti wote wa vitongoji vya kata hiyo.1
Aidha Diwani huyo aliwaarika viongozi wastaafu amval ni azee wa mkwese, ili kurahisisha zoezi ambapo mmoja ya wawakilishi wa wazee hao ambae ni mwenyekiti Mstaafu wa kijiji cha Kinyika, Mzee lupaa (87), amemshukuru Diwani Shigela kutenga siku moja ya kila wiki kupokea, kusikiliza na kutatua kero za watu wa kata ya Mkwese kuwa ni chachu katika kuwaletea maendeleo watu wa mkwese.

Kliniki hiyo itakuwa ikifanyika kila siku ya Alhamisi ya kila wiki kuanzia saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 10:00 Jioni.
Discussion
Reader comments
0 contributions