Skip to main content

NFRA YATAKIWA KUHARAKISHA MAUZO YA MAZAO

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuharakisha taratibu za kuuza mazao pindi masoko yanapopatikana, ili kuepuka kupoteza fursa hizo kutokana na michakato mirefu.

NFRA YATAKIWA KUHARAKISHA MAUZO YA MAZAO

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameitaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuharakisha taratibu za kuuza mazao pindi masoko yanapopatikana, ili kuepuka kupoteza fursa hizo kutokana na michakato mirefu.

Vilevile, amezitaka taasisi zinazohusika kuendelea kutafuta masoko ya kudumu na kuwezesha uuzaji wa mazao nje ya nchi, huku akieleza kuwa bei ya kununua mahindi kupitia NFRA imeongezwa kutoka shilingi 450 hadi shilingi 500.

Amesema hayo Bungeni, jijini Dodoma leo (Alhamisi, Novemba 05, 2026), wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, katika Mkutano wa Tano, Kikao cha Nane cha Bunge la 13.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kongwa, Isaya Mngurumi Moses, aliyetaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kutafuta masoko na kuboresha bei za mazao ili wakulima wanufaike na uzalishaji wao.

Dkt. Mwigulu amesema NFRA inapopata masoko inapaswa kukamilisha taratibu za mauzo kwa wakati, kwa sababu ucheleweshaji unaweza kuwafanya wanunuzi kupata mazao katika masoko mengine yenye michakato mifupi zaidi.

Amesema Serikali imekuwa ikitumia mazungumzo na viongozi wa mataifa mbalimbali kutafuta masoko ya mazao ya Tanzania na kupanua wigo wa biashara kwa wakulima.

Kuhusu bei ya mahindi, Waziri Mkuu amesema amekutana na Wizara yenye dhamana ya kilimo mara kadhaa kujadili namna ya kuboresha bei ya ununuzi kupitia NFRA.

Amesema bei hiyo iliongezwa kutoka shilingi 200 hadi shilingi 300, baadaye shilingi 450 na sasa shilingi 500.

“Tulikaa tena kwa mara ya mwisho, tukashauriana kwamba kama bado wanaweza kwenda juu zaidi, wafanye hivyo, na tulikubaliana sasa watapeleka iwe shilingi 500,” amesema.

Amewataka wakulima wenye mahindi wanayohitaji kuuza kufika katika ofisi za NFRA za mikoa na kanda ili kutumia fursa ya bei hiyo iliyoboreshwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.