Na Adam Mbilinyi.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza rasmi dhamira yake ya kuipiundua Serikali ya Jamhuri ya kiislam, Iran.
Katika taarifa yake, Netanyahu amebainisha kuwa, atauangusha utawala huo.
Ameeleza kuwa, “utawala wa Iran ni dhaifu kuliko wakati wowote ule na unafanya kila unachoweza ili kusalia mamlakani."
Akiwa katika hafla maalum iliyowakutanisha viongozi wa kijeshi, Netanyahu amedai kuwa ana imani ya kuwapo kwa uwezekano wa kuondoa tishio la Iran.

Kuhusu Iran kutoilenga Israel katika mashambulizi ya hivi karibuni, Netanyahu amebainisha kwamba haikuwa bahati mbaya na inafahamu vyema nguvu, silaha na azimio kuu la Israel.
Kauli ya Netanyahu, inakuja wakati ambapo upinzani unazidi kuongezeka nchini Israel, huku ikijiandaa kuelekea katika duru ya Uchaguzi wa Bunge la 26 “kneesset” Oktoba 27, 2026.
Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema nchi yake iko tayari kujibu kwa nguvu kubwa iwapo Iran itashambulia wakati wa sikukuu za Kiyahudi nchini Israel, zinazoanza katikati ya mwezi wa Septemba.
Amesema, Iran ililenga mashambulizi mbalimbali katika eneo hilo, isipokuwa Israel, wakati wa mzozo wa hivi karibuni.
Discussion
Reader comments
0 contributions