Skip to main content

NETANYAHU ATAKAMATWA MARA MOJA: KOREA KUSINI

Ni kauli iliyoibua utata iliyotolewa na Rais wa Koresa kusini Lee Jae-myung, akisema Israel imevuka mstari mwekundu Chini ya masharti ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) na kwamba Waziri mkuu wa Israel Benjamin Benzion Netanyahu atakamatwa mara moja tu atakapokanyaga katika ardhi ya Korea Kusini.

NETANYAHU ATAKAMATWA MARA MOJA: KOREA KUSINI
Studio Narration JAMBO FM

NETANYAHU ATAKAMATWA MARA MOJA: KOREA KUSINI

0:00 --:--

Ni kauli iliyoibua utata iliyotolewa na Rais wa Koresa kusini Lee Jae-myung, akisema Israel imevuka mstari mwekundu Chini ya masharti ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) na kwamba Waziri mkuu wa Israel Benjamin Benzion Netanyahu atakamatwa mara moja tu atakapokanyaga katika ardhi ya Korea Kusini.

Kauli hiyo ya Rais wa Korea kusini inakuja kufuatia hatua za hivi karibuni zinazotajwa kuharibu diplomasia za mataifa hayo ikiwemo Kuwakamata kwa Wanaharakati.

Jeshi la majini la Israel lilifanya oparesheni ya kuikamata meli ya msaada (Gaza flotilla) iliyokuwa ikielekea Gaza. Ndani ya meli hiyo kunaarifiwa kulikuwamo na raia wawili ambao ni wanaharakati wa Korea Kusini ambao walikamatwa na kuwekwa kizuizini na Israel.

Kufuatia hatua hiyo na matamshi ya utata ya Netanyahu Msimamo wa Rais Lee Jae-myung wa Korea kusini uliibuka katika kikao cha Baraza la Mawaziri nchini Korea Kusini Rais Lee Jae-myung alionesha kukasirishwa na hatua hiyo ya Israel akimwita Netanyahu “mhalifu wa vita".

Korea Kusini ni nchi mwanachama wa Mkataba wa Rome ulioanzisha ICC, ambayo kisheria ina wajibu wa kushirikiana na mahakama hiyo katika amri za kuwakamata watuhumiwa zinapotolewa.

Hata hivyo ICC ilitoa hati ya kumkamata Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, pamoja na viongozi wengine kwa tuhuma za makosa ya vita na dhuluma dhidi ya binadamu huko Gaza.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.