Skip to main content

'NENO LA MWISHO': WATANZANIA PAMBANENI KUPATA KATIBA MPYA - MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema endapo angepata nafasi ya kutoa neno moja la mwisho kwa Watanzania, angewataka wapambane kupata Katiba Mpya.

Dkt. Nchimbi ameyqswmq hayo hii leo Julai 24, 2026 Jijini Dar es salaam, katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu.

Amesema, “kama nina kitu cha kuwaambia Watanzania, ningewaambi pambaneni mpate Katiba Mpya itakayodumu miaka 50, yenye mwafaka katika Taifa, itakayotupeleka mbele miaka 50.”

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Balozi Dkt.Nchimbi amebainisha kwamba, mjadala wa kupata Katiba Mpya umedumu kwa zaidi ya miaka 40, na kwamba vuguvugu la kuitafuta lilianza rasmi mwaka 1992.

Aidha, amesema, Serikali ya Awamu ya Nne ilianza mchakato wa Katiba Mpya, lakini changamoto iliyojitokeza ni kuwa madai ya Wananchi yalikuwa mengi na yalihitaji kushughulikiwa kwa pamoja.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.