Skip to main content

NECTA YATANGAZA MATOKEO KIDATO CHA SITA, KUNA ONGEZEKO LA UFAULU

Baraza la Mitihani Nchini (NECTA), limetangaza matokeo ya Kidato cha sita na Mitihani ya Ualimu ya Mei 2026, yakionyesha ongezeko la kiwango cha ufaulu ambapo watahiniwa wa shule wamefaulu kwa asilimia 99.92.

NECTA YATANGAZA MATOKEO KIDATO CHA SITA, KUNA ONGEZEKO LA UFAULU

Baraza la Mitihani Nchini (NECTA), limetangaza matokeo ya Kidato cha sita na Mitihani ya Ualimu ya Mei 2026, yakionyesha ongezeko la kiwango cha ufaulu ambapo watahiniwa wa shule wamefaulu kwa asilimia 99.92.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Ally Mohamed amesema, kati ya watahiniwa 125, 320 wa shule waliopata matokeo, 125,056 wamefaulu kwa kupata madaraja ya Kwanza, pili, tatu na nne, huku Watahiniwa wa kujitegemea, waliofaulu ni 6,012, sawa na asilimia 94.

Aidha, Watahiniwa 124,663, sawa na asilimia 99.6, walipata daraja la kwanza, pili na tatu, hali inayoonesha kuwa ubora wa ufaulu umeendelea kubaki zaidi ya asilimia 99 kwa miaka minne mfululizo.

Idadi ya watahiniwa waliopata Daraja la kwanza imeongezeka kutoka 61,020 mwaka 2025, hadi 67,606 kwa mwaka 2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.5. Daraja la Kwanza sasa linawakilisha asilimia 54.11 ya watahiniwa wote waliopata matokeo.

Kwa upande wa jinsia, wasichana waliofaulu ni 61,703, sawa na asilimia 99.94, huku wavulana waliofaulu wakiwa 63,323, sawa na asilimia 99.91, jambo linaloonyesha kuwa tofauti ya ufaulu kati ya jinsia hizo ni ndogo.

Katika mchepuo wa sayansi asilia, watahiniwa 38,118 walipata madaraja ya Kwanza na Pili, wakilinganishwa na 37,677 mwaka 2025 na 31,386 mwaka 2024. Mchepuo wa Historia, Kiswahili na Lugha (HKL) uliongoza kwa kuwa na zaidi ya asilimia 95 ya watahiniwa waliopata Daraja la Kwanza na Pili.

Kwa upande wa shule, kati ya 1,064 zilizokuwa na matokeo, shule 757, sawa na asilimia 71, zilipata wastani wa Daraja C, huku shule 943, sawa na asilimia 88, zikipata wastani wa Daraja A hadi C, huku kukiwa hakuna shule iliyopata wastani wa Daraja F mwaka 2026.

Kuhusu ufaulu wa masomo, yote yalikuwa na kiwango cha ufaulu cha zaidi ya asilimia 93. Somo la Basic Applied Mathematics (BAM) ndilo lililokuwa na ufaulu wa chini zaidi wa asilimia 80.5, lakini kuna ongezeko kutoka asilimia 73 mwaka 2025.

Jumla ya watahiniwa 133,647 walijiandikisha kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita katika vituo 2,992 nchini, ambapi kati yao Wasichana nu 65,217 na Wavulana 68,491 huku mahudhurio ya watahiniwa wa shule yakiwa asilimia 99.22 na watahiniwa wa kujitegemea asilimia 91.35.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.