Skip to main content

NDOTO, ADUI CHANZO KIUNGANISHI CHA URAFIKI WA NYERERE, MANDELA

Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi mzalendo wa Afrika Kusini Nelson Mandela wanatajwa kuwa urafiki mkubwa uliochagizwa na adui mmoja, wakiwa na ndoto moja,

NDOTO, ADUI CHANZO KIUNGANISHI CHA URAFIKI WA NYERERE, MANDELA
Studio Narration JAMBO FM

NDOTO, ADUI CHANZO KIUNGANISHI CHA URAFIKI WA NYERERE, MANDE...

0:00 --:--

Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi mzalendo wa Afrika Kusini Nelson Mandela wanatajwa kuwa urafiki mkubwa uliochagizwa na adui mmoja, wakiwa na ndoto moja,

Waazee hawa hawakuwa marafiki wa kawaida wa kukutana kwenye sherehe, kwani urafiki wao ulijengwa kwenye damu na mapambano ya ukombozi wa Afrika.

Zipo sababu nne ambazo kwa leo nazianisha, zilizochangia kuufanya autafukiwa kuwa imara.

1. Nyerere alipigania uhuru wa Mandela.

Mandela akiwa gerezani Robben Island kwa miaka 27, Nyerere alikuwa sauti yake kubwa zaidi duniani.

Tanzania ndiyo ilikuwa mstari wa mbele wa kupinga ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini - Apartheid. Nyerere alikataa kabisa kufanya biashara na serikali ya makaburu hadi Mandela aachiwe.

2. Tanzania ilikuwa nyumbani kwa ANC.

Wakati ANC ya Mandela ilipigwa marufuku Afrika Kusini, Nyerere aliwapa makazi Dar es Salaam. Morogoro ndiko ANC ilifanyia mkutano wake mkubwa wa kwanza wa kimkakati 1969. Wapiganaji wa Umkhonto we Sizwe walipata mafunzo na silaha kupitia Tanzania.

Mandela mwenyewe alisema: _"Bila Tanzania, kupigania uhuru wa Afrika Kusini kusingewezekana."

3. Wote waliamini Umoja wa Afrika.

Wote wawili hawakuamini uhuru wa nchi moja tu. Nyerere aliita "Uhuru si kamili hadi Afrika yote iwe huru". Mandela aliishi hivyo hivyo. Ndio maana Nyerere alitoa uchumi mdogo wa Tanzania kusaidia vita vya ukombozi Msumbiji, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini.

4. Waliheshimiana kama baba na mwana.

Nyerere alikuwa mkubwa kwa Mandela kwa miaka 4. Mandela alimwona Nyerere kama mwalimu na baba wa ukombozi. Nyerere alimwona Mandela kama uthibitisho kwamba mapambano yake hayakuwa bure.

Ndiyo maana kwenye picha hii, Nyerere anaongea kwa mikono yote, Mandela anamsikiliza kwa heshima. Si marafiki wa siasa tu, ni ndugu wa mapambano.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.